Maneno ya Mwokozi: “Leo niletee mapadri wote na watawa. Uwazamishe katika kilindi cha huruma yangu isiyo na mwisho. Ni wao hasa walionipa nguvu ya kuweza kuyavumilia mateso yangu makali mno. Kwa njia yao, kama vile mifereji, huruma yangu humiminika na kuwatiririkia wote.”
Kiongozi: Tuwaombee mapadri wote na
watawa ili wadumu kiaminifu katika utumishi wao na wakfu wa maisha yao kwa Yesu
Kristo Bwana harusi wao.”
Wote: Ee Yesu mwenye huruma tele,
kwako hutoka mema yote. Uwazidishie neema yako watawa wanawake waliojitolea na
kuwekwa wakfu katika utumishi wako, ili watekeleze utumishi wao kwa huruma na
kwa jinsi inayofaa, na kwamba wale wanaowaona na kuzishuhudia kazi zao bora,
waweze kumtukuza Baba wa Huruma aliye mbinguni. Amina.
Baba yetu …….
Salamu Maria …… Atukuzwe ……
Kiongozi: Tuwaombee mapadri na watawa
wote ambao ni vyombo vya huruma ya Mungu.
Wote: Baba wa Milele, elekeza macho
yako yenye huruma, juu ya jeshi teule la wafanyakazi shambani mwako. Uzitazame
kwa wema roho zao mapadre na watawa wote. Uwajalie wingi wa Baraka zako. Kwa
njia ya upendo wa Moyo wa Mwanao, humo ambamo wameingizwa, uwape nguvu na
mwanga, ili waweze kuwaongoza wengine katika njia ya wokovu, na kwa sauti moja,
waihimidi huruma yako kwa nyimbo za sifa bila mwisho. Amina.
No comments:
Post a Comment