NAMNA YA KUSALI ROZARI YA HURUMA
Tumia Rozari ya kawaida na anza kwa kusali ishara ya msalaba (+)
Baba Yetu…
Salam Maria 3
Nasadiki…
Penye Punje Kubwa
Baba wa Milele, ninakutolea Mwili na Damu. Roho na Umungu wa Mwanao Mpenzi sana Bwana Wetu Yesu Kristu, kwa kuzilipia dhambi zetu na dhambi za dunia nzima.
Penye Punje ndogo
K : Kwa ajili ya mateso makali ya Bwana
Yesu Kristu, x 10 (50)
W: Utuhurumie sisi na dunia nzima x 10 (50)
Mwisho sali mara tatu
MUNGU MTAKATIFU, MTAKATIFU MWENYE ENZI, , MTAKATIFU UNAYEISHI MILELE, UTUHURUMIE SISI NA DUNIA NZIMA.
LITANIA YA HURUMA YA MUNGU
Bwana utuhurumie
Kristo utuhurumie
Bwana utuhurumie
Kristo,utusikie
Kristo utusikilize
Baba wa mbinguni Mungu Utuhurumie ( iwe kiitikio)
Mwana Mkombozi wa dunia
Roho Mtakatifu Mungu
Utatu mtakatifu Mungu mmoja
Huruma ya Mungu iliyosifa kuu ya muuumna
wetu
Tunakutumainia (iwe kiitikio)
Huruma ya Mungu iliyo kilele cha ukamilifu
wa mwokozi wetu
Huruma ya Mungu iliyo upendo usiopimika wa Roho Mtakasa
Huruma ya Mungu iliyofumbo
lisilofdahamika la utatu matakatifu
Huruma ya Mungu iliyoishara ya uwezo mkuu
wa Mungu mwenyezi
Huruma ya Mungu iliyofumbuliwa katika
kuziumba roho za malaika wa mbiguni
Huruma ya Mungu iliyotuumba na kutuamuru
tuwepo bila kutokana na chochote
Huruma ya Mungu inayoshika na kushikiza
ulimwengu mzima
Huruma ya Mungu inayotujalia maisha ya
kuto kufa
Huruma ya Mungu inayotukinga na adhabu
tunazostahili
Huruma ya Mungu inayotuinua tutoke katika
taabu, unyonge na maumivu ya dhambi zetu
Huruma ya Mungu inayotufanya wenye haki, katiuka Neno Aliyejifanya Mtu
Huruma ya Mungu inayofurika kutoka katika
majeraha ya Kristu
Huruma ya Mungu inayobubujika toka ndani
ya moyo mtakatifu wa Yesu
Huruma ya Mungu iliyotupatia Bikira Maria
mtukufu kabisa, awe kwetu “Mama wa Huruma”
Huruma ya Mungu inayoonyeshwa katika
Ufunuo wa Mafumbo Matakatifu ya Mungu
Huruma ya Mungu iliyoonyeshwa katika
kuanzishwa Kanisa Katoliki
Huruma ya Mungu inayopatikana katika
mafumbo ya Sakramenti Takatifu
Huruma ya Mungu inayotolewa kwa wanadamu
wote, kwa njia ya Sakramenti ya Ubatizo na Kitubio
Huruma ya Mungu inayotolewa katika
Sakramenti ya Ekaristi na ya Upadrisho
Huruma ya Mungu inayoonyeshwa kwetu pale
inapotuita na kutuingiza katika kuwatakatifuza wenye haki
Huruma ya Mungu inayotimilika katika
ukamilifu wa watu watakatifu
Huruma ya Mungu chemchemi ya afya kwa
wagonjwa na wote wanaoteseka
Huruma ya Mungu iliyo faraja ya wote
wenye uchungu moyoni
Huruma ya Mungu iliyo tumaini la roho
zinazosumbuliwa na mkato wa tamaa
Huruma ya Mungu iliyo mwenzi wa daima na
popote wa watu wote
Huruma ya Mungu inayowahi kutuletea neema
zake
Huruma ya Mungu iliyo amani yao wanaokufa
Huruma ya Mungu iliyo burudisho na faraja
yao marehemu toharani
Huruma ya Mungu iliyo furaha ya mbinguni
kwa watakatifu wote
Huruma ya Mungu iliyo taji la watakatifu wote
Huruma ya Mungu chemchemi ya miujiza isiyokauka
Mwanakondoo wa Mungu uliyetuonyesha Huruma
yako Kuu katika kuikomboa dunia kwa Msalaba wako Mtakatifu,
Utusamehe Ee Bwana
Mwanakondoo wa Mungu unayejitolea kwetu
kwa mapendo na Huruma katika kila Adhimisho la Sadaka ya Misa Takatifu
Utusikilize Ee Bwana
Mwanakondoo wa Mungu unayeondoa dhambi ya
dunia kwa njia Huruma Yako isiyo na mwisho
Utuhurumie
V: Bwana, utuhumie
R: Kristu, utuhurumie
W: Bwana, utuhurumie.
V: Huruma anana za Bwana zi juu ya kazi
zake zote.
R: Huruma za Bwana nitaziimba milele.
TUOMBE
Ee Mungu uliye na huruma isiyo na mwisho na hazina za wema na upendo wako, hazina mipaka. Tunakusihi ututazame sisi watu wako huku duniani na kutuongezea Huruma Yako tena na tena, ili itusaidie, tusije tukakata tamaa hata mara moja, haidhuru, tukumbane na majaribu makubwa kiasi gani, bali tuweze daima kuzielekea na kuzishika Amri zako kwa matumaini na kutimiza Mapenzi yako Matakatifu, ambayo ndiyo”Huruma yenyewe”. Tunaomba hayo kwa njia ya Bwana wetu Yesu Kristu Mwanao, Mfalme wa Amani na Huruma, aishie na kutawala Nawe, na Roho Mtakatifu kwa pamoja mkituonyesha Huruma, daima na milele. Amina
Safi iko vizuri
ReplyDelete