SALA YA KUJIZAMISHA KATIKA HURUMA YA MUNGU NA KUMWABUDU YESU ALIYEZIMIA MSALABANI SAA TISA - GG Resource

LEARNING & ENTERTAINMENT

Saturday, November 14, 2020

SALA YA KUJIZAMISHA KATIKA HURUMA YA MUNGU NA KUMWABUDU YESU ALIYEZIMIA MSALABANI SAA TISA

SALA

Ee mkombozi wangu Yesu Kristo, ninakuabudu wewe uliyezimia juu  msalabani, kwa kunipenda mimi na watu wote duniani. Ninakushukuru kwa kuwa ulikufa na kutukomboa kwa Msalaba  wako Mtakatifu.

Ee Mungu Baba wa milele, ninakutolea mwanao mpenzi, Bwana wetu Yesu Kristo; aliyewambwa Msalabani, akavuliwa nguo, akapondwa kwa mapigo, akapigiliwa taji la miiba kichwani, akatobolewa kwa misumari mikononi na miguuni, akachomwa ubavuni kwa sime (mkuki mkubwa) mwili mzima ukalowa Damu.

Ee Mungu wangu, mwenyewe huyo ni mwanao mpenzi, ndiye ninayekutolea, nikiwa katika hali ya uchungu na majuto ya moyo.

Baba mwenyezi, pokea sadaka takatifu ya mwanao Yesu Kristo, aliye thamani ya ukombozi wetu. Ni Damu ya Mungu halisi ninayokutolea, kwa kuzilipia dhambi zangu, za ndugu na jamaa zangu, na za watu wote duniani, kuwapatia faraja marehemu wa Toharani, kwa kuzituliza roho zenye taabu na huzuni, kwa ajili ya wale wanaodhulumiwa, kwa faraja yao wagonjwa, kwa wale walio katika hatari ya kufa, kwa wokovu Wao watakaofariki dunia Leo. Ninakutolea pia kwa ajili ya uongofu wa wakosefu masikini, uongofu wangu Mimi, wa wenzangu na wa jamaa zangu. Ninakuomba uwaimarishe wakristo wote wema na kufanikisha ustawi na maendeleo ya Dini yetu Katoliki. Utujalie sote Huruma yako, hali njema na baraka yako juu ya kazi zetu, utujalie afya ya roho na mwili. Hayo yote yawe kwa sifa yako, heshima na utukufu wako nyakati zote. Umjalie kila mmoja wetu na watu wote, kufikia ule ukamilifu ulio kadiri ya azimio lako la milele.

Tunamuombea baba Mtakatifu wetu……………., Maaskofu wote na Mapadri. Wakubwa wetu, Watawa wote waume kwa wake, Familia zote za Kikristu, Vijana wavulana kwa wasichana, Watoto wote wadogo, Viongozi wote wa serikali. Tunawaombea wafadhili wetu wote wa roho na mwili na ulimwengu wote kiujumla.

Utujalie sisi sote kuishi maisha mema ya Utakatifu na mwishowe utujalie kifo Chema na Heri isiyo na mwisho huko Mbinguni. Amina


Imeandaliwa na Ginas Ngowi 

(Kitabu cha Huruma ya Mungu, Mt. Faustina)

1 comment:

ABOUT US

This website is concerned with social,spiritual and science articles,purposely to share with others those which can be learnt
'; (function() { var dsq = document.createElement('script'); dsq.type = 'text/javascript'; dsq.async = true; dsq.src = '//' + disqus_shortname + '.disqus.com/embed.js'; (document.getElementsByTagName('head')[0] || document.getElementsByTagName('body')[0]).appendChild(dsq); })();