JINSI YA KUFANYA NOVENA YA HURUMA
YA MUNGU
Anza Novena hii siku ya Ijumaa Kuu kwa siku tisa (unamaliza
Novena kabla ya Jumapili ya kwanza baada ya Pasaka, “Jumapili ya Huruma ya
Mungu”). Lakini unaweza kufanya Novena hii wakati wowote mwakani, isipokuwa
Novena ianzwe katika siku ya Ijumaa.
Kila siku anza kwa kusali sala hizi kama ifuatavyo pamoja
na sala ya siku husika hapo chini, sala ya siku ndio itakayobadilika tu kwa
kila siku kwa hiyo sala hizi zingine utasali kama kawaida kila siku
Anza kwa kusali Sala zifuatazo
1. Uje Roho
Mtakatifu:
Uje Roho Mtakatifu, uzienee nyoyo za waamini wako, washa
mapendo yako, peleka Roho wako, vitaumbwa upya na nchi zitageuka.
Tuombe; Ee Mungu uliyefundisha nyoyo
za waamini wako, ukiwaletea mwanga wa Roho wako Mtakatifu, tunakuomba utuongoze
na Yule Roho, tupende yaliyo mema, tupate daima faraja zake, tunaomba hayo kwa
njia ya Kristo Bwana wetu, Amina.
2. Sala ya Kutubu
Mungu wangu, ninatubu sana dhambi zangu, kwani ndiwe mwema,
ndiwe mwenye kupendeza, wachukizwa na dhambi, basi sitaki kukosa tena,
nitafanya kitubio, naomba neema yako nipate kurudi kwako, Amina.
3. Weka Nia za Sala
Kila siku ya Novena soma maneno ya Bwana Yesu kwa kuweka
nia ya sala za siku hiyo, na pia Sali sala fupi kuhusu nia husika kama
zilivyoonyeshwa hapo chini, kisha; Hapa ndipo utasali sala za kila siku, mfano,
siku ya kwanza utasali Sala ya Siku ya kwanza, siku ya pili sala ya siku ya
pili na kuendelea mpaka siku ya tisa.
No comments:
Post a Comment