HISTORIA YA MENGI KWA UFUPI
Reginald Mengi alikuwa kati ya wafanyabiashara maarufu hapa Tanzania pamoja na Afrika mashariki kwa ujumla, umaarufu wake unatokana na juhudi zake za kushiriki mambo mbaliambali ya kijamii hasa kusaidia watu wasiojiweza mfano yatima, walemavu, wajane na watu wa kipato cha chini.
Reginald Mengi alikuwa kati ya wafanyabiashara wenye ushawishi mkubwa sana hapa Tanzania kutokana na kuwa mstari wa mbele kukemea maovu ndani ya jamii.
Dr. Reginald Mengi alizaliwa mkoani Kilimanjaro wilaya ya Machame katika familia ya kipato cha chini. Wakati akisoma shule alikuwa anafikia hatua ya kwenda shule bila viatu huku yeye na wazazi wake walikuwa wanaishi nyumba moja na mbuzi pamoja na Ng’ombe kutokana na familia yao kuwa na uwezo mdogo kifedha.
Reginald Mengi alikuwa na tabia nzuri kipindi cha ujana wake. Hakuwahi kuhusishwa na kesi shuleni au mtaani maana wazazi wake walimlea kwenye maadili ya dini kwa hiyo hali hiyo ilimsaidia Mengi kuwa na tabia njema mbele ya Jamii.
Reginald Mengi alipata elimu ya sekondari katika shule ya Moshi sekondari au zamani OLD MOSHI baada kumaliza shule ya sekondari alipata ufadhili (sponsorship). Alikwenda Uingereza kuchukua masomo ya uhasibu. Dr. Reginald Mengi ni moja kati ya watanzania wa mwanzo kabisa kusoma UK, Scotland na kufanikiwa kuwa Mhasibu anayetambulika na Taasisi ya Wahasibu ya Uingereza na Walesi
Mwaka 1971 Reginald mengi alirudi Tanzania na kuajiriwa kwenye kampuni ya Cooper and Lybrand Tanzania ambayo kwa sasa inajulikana kama Prince water house Cooper. Baada ya kufanya kazi muda mrefu kwenye kampuni hiyo akiwa kama chairman and partner mwaka 1989 aliondoka kwenye kampuni hiyo na kwenda kuanzisha kampuni yake. Dr. Reginald Abraham Mengi ni mwanzilishi, mmiliki na Mwenyekiti mtendaji wa makampuni ya IPP Limited na Taasisi ya teknolojia na ugunduzi ya IPP(IPP Institute of Technology and Innovation).
Reginald Mengi wakati akianzisha IPP MEDIA GROUP ilikuwa ni kampuni ndogo sana ambayo alianza kwa kutengeneza kalamu za wino lakini IPP MEDIA GROUP iliendelea kupanuka na kwa sasa ni kati ya makampuni makubwa hapa Afrika mashariki kwa ujumla.
Kupitia kampuni yake hiyo Reginald Mengi aliweza kumiliki vyombo mbalimbali vya habari mfano kwa upande wa TV alimiliki ITV, EATV na Capital Tv na kwa upande wa Radio anamiliki Radio one, Capital radio na EATV radio. Dr. Reginald Mengi alimiliki magazeti kadhaa, mfano wa magazeti hayo ni Nipashe, kulikoni, Taifa letu , The Guardian , Financial time na Sunday observer.
Reginald Mengi alimiliki viwanda baadhi ambavyo vinazalisha vinywaji mbalimbali hapa Tanzania. Alimiliki viwanda vya kutengeneza vinywaji.Vinywaji hivyo ni maji ya Kilimanjaro ambayo ndiyo maji yenye ubora zaidi. Pia viwanda hivyo vinazalisha soda mfano cocacola, Fanta & Tangawizi.
Na Leo mauti inamkuta akiwa Dubai Bwana ametoa na Bwana ametwaa jina lake lihimidiwe... Apumzike kwa Amani..
Na .....J.shao
No comments:
Post a Comment